Muktadha wa Kijiografia
Uzingativu wa Miteremko ya Kimwinuko

Uchunguzi kuhusu mfumo wa kutegemeana kati ya nyanda za juu na tambarare

Utafiti shirikishi wa kimataifa wa LKCCAP umelenga kutafiti mifumo ya uhusiano kati ya nyanda za juu na tambarare katika Mkoa wa Kilimanjaro (angalia ramani ya mkoa). Uchunguzi wa awali wa timu ya LKCCAP unadokeza kwamba mtiririko wa maarifa, nguvu kazi, mitaji ya kifedha, bidhaa, na mifugo kati ya juu na chini kufuatia miteremko-mwinuko unaweza kupanua mibadala ya riziki za wakaazi, kuongeza uwezo wa ujihimilishaji, na kuingiliana na asasi za ngazi ya jumuiya. Tunafanya uchunguzi kuhusu jinsi gani michakato hii inavyoathiri mienendo ya kijamii ya upatikanaji na utumizi wa maliasili na mbadaliko ya maarifa-enyeji hususan katika muktadha wa mabadiliko ya tabianchi na mabadiliko ya kimazingira kwa ujumla. Uchunguzi wa maarifa-enyeji kama kijenzi cha ujihimilishaji wa muda mfupi na muda mrefu unaweza kubainisha mlolongo wa mikakati ya ki-spashia inayobuniwa na jumuiya zinatofautina kijamii.