Kiunzi cha Mbinu za Utafiti
GIS Shirikishi & Mkabala wa Mbinu Mseto wa Ukusanyaji wa Taarifa na Uchambuzi

Uchambuzi katika ngazi anuai

Modeli-igizi za sasa za mabadiliko ya tabianchi hutoa utabiri na kubaini mandhari-dhahania ambayo ni muafaka kwa mipango na tathmini katika ngazi za kidunia na kiukanda. Ngazi hiyo ya kina cha taarifa si toshelevu kwa kupata ufahamu wa kina wa athari za mabadiliko ya tabianchi katika ngazi za jumuiya/jamii ndogondogo. Mintaarafu hoja hii, watafiti  wa LKCCAP wanakusudia kujumuisha taarifa za aina mbalimbali na kutumia mbinu mseto za kukusanya taarifa ili kujenga ufahamu ulioegemea vyanzo na mbinu mbalimbali kuhusu mikakati ya ujihimilishaji katika kupata riziki katika. Mkoa wa Kilimanjaro nchini Tanzania.


Umuhimu wa ushiriki wa jumuiya

Utafiti huu unachunguza michango na mipaka ya mifumo tofauti ya maarifa-enyeji kimwenendo na kijamii katika uwezo wa ujihimilishaji, na pia unachambua kwa jinsi gani asasi katika ngazi ya jumuiya zinavyoweza kuboresha, kuzorotesha, na kuleta mageuzi katika maarifa-enyeji. Mbinu za utafiti wa uwandani zinazotumiwa na LKCCAP zilibainishwa kwa misingi wazi ya kuzingatia kiunzi shirikishi ambacho kinajumuisha fikira na maoni kutoka kwa watafiti na wanajumuiya katika kila hatua ya mradi huu.


Kiunzi GIS (PGIS) shirikishi

Mojawapo ya lengo kuu la LKCCAP ni kutengeneza ramani ambapo inatumia mbinu za kawaida za PRA na pale inapofaa inatumia teknolojia ya jiospashia na kanuni za kinadharia za sayansi ya GIS katika kupembua viwango na vipengee anuai vya kijiografia kuhusiana na uwezo wa ujihimilishaji kijiografia-jamii. Mojwapo ya shughuli kuu ya utafiti katika mradi huu ni pamoja na utengenezaji wa PGIS ili kujumuisha na kuchambua tarifa uchunguzi wa uwandani , takwimu na data za spashia, na vile vile matokeo ya ufananishi wa tabianchi:

  • Udodosaji taarifa za kaya. Jumla ya Kaya 650 katika maeneo teule ya ukanda wa juu, ukanda wa kati, na ukanda wa chini (tambarare) katika miteremko-miinuko minne iliyomo katika ukanda wa Pare-Kilimanjaro ziliteuliwa kama sampuli nasibu katika mwaka wa 2010 ambapo taarifa zilidodosolewa kuhusu mikakati ya kutafuta riziki na mitazamo ya wakulima na wafugaji kuhusu mabadiliko ya kimazingira katika jumuiya zao. Pia inawezekana kwa kiasi fulani kuchunguza jinsi gani maarifa ya mabadiliko ya tabianchi katika upana mkubwa katika ngazi za ukanda na dunia yanavyoathiri mitazamo ya ngazi za jumuiya/jamii ndogondogo.
  • Majukwaa ya jumuiya shirikishi. Mikutano kadhaa imeandaliwa kufanyika katika mwaka wa 2010-2011 ili kufanya tathmini juu ya: viashiria muafaka kuhusu uwezo wa ujihimilishaji kijiografia-jamii; mienendo ya ujihimilishaji wa riziki ya muda mfupi na muda mrefu ndani ya kaya na kati ya kaya na kaya; na mawanda ya kiutamaduni na kiisimu ya mitazamo na mijadala juu ya mabadiliko ya tabianchi.
  • Warsha za Uchoraji Ramani (PRA). Warsha kadhaa zitaendeshwa katika kila jumuiya ambamo washiriki watatengeneza ramani za riziki, mandhari za kimazingira, kiasasi, na kiisimu-jumuiya kwa kutumia muundo-huria wa uchoraji na ramani za vijiji zilizomo tayari katika jumuiya.
  • Miradi ya Utafiti Inayoratibiwa na Jumuiya. Miradi shirikishi inayoratibiwa na jumuiya itashughulikia ukusanyaji wa uwandani wa taarifa za kimazingira, mbinu za taarifa katika ujumla wake(k.m., kukurekodi maongezi juu ya mabadiliko) na kutumia GPS kuweza kuchora mandhari ya kimazingira na kijamii ambayo yanadhihirisha dhima ya maarifa-enyeji katika ujihimilishaji.
  • Majukwaa ya Wadau. Warsha za kujenga mandhari-dhahania zitaendeshwa kuelekea mwisho wa mradi huu ili kutafakari na kuzingatia vipengele muhimu vya data iliyokusanywa katika kipindi chote cha mradi na kuchunguza athari za kimazingira na kijamii ziwezazo kujiibusha katika ujihimilishaji. Timu ya watafiti itashirikiana na wadau katika asasi husika kutengeneza upembuzi yakinifu wa gharama na kimazingira kuhusiana na mitupo (trajectories) ya ujihimilishaji.

PGIS pia itaweza kuboresha shughuli shirikishi za kujifunza ambazo zitafanywa katika kipindi chote cha mradi. Itaweza kupembuliwa ili itumike kama kifaa-fananishi katika mtandao wa kompyuta kwa ajili ya watafiti katika timu ya LKCCAP kuendelea kubadilishana mawazo na watengeneza sera, asasi za kijamii, na pia kama kifaa cha elimu kwa kutumiwa na vyuo vikuu vya Marekani na Tanzania.


Utafiti wa GIS wa media-mseto, utengenezaji wa mandhari-dhahania, na Utengenezaji wa Mitaala

Watafiti wa LKCCAP watatumia na kuzingatia vyanzo vyote vya taarifa vilivyotajwa hapo juu kwa ajili ya uchambuzi na utengenezaji ramani wa uwezo wa ujihimilishaji katika viwango mseto. Mradi huu utatengeneza mfumo wa taarifa za kifiografia –GIS wenye media-mseto ambao utajumuisha data za kawaida za vekta  na spashia- rasta na zile za  zilizosimbuliwa kijiografaia pamoja  na  mediamseto.  Mfumo huo utatumiwa kuibua welewa mpya juu ya kuunganisha viunzi vya kiuchanganuzi vya taarifa za jumla na za kitakwimu za Sayansi ya GIS ili kujenga msingi wa utafiti wa ujihimilishaji unaochochewa na mabadiliko ya tabianchi.

GIS ya media-mseto pia itakuwa na jukwaa kwa kujengea vitengo (modules) kwa ajili ya kubadilishana data za jiospashia  na kutengeneza taarifa zitokanazo na ramani ili kuwasilisha kwa hadhira pana matokeo muhimu ya utafiti. Seti ndogo ya vipengele vya GIS ya multimedia itakuwa imefungamanishwa katika tovuti ya mradi huu kwa kutumia teknolojia ya utengenezaji ramani kwa njia ya mtandao ili kuwezesha kufikisha tarifataarifa muhimu kwa watumiaji wengine nje ya timu ya watafiti, na pia kuwawezesha watafiti wengine kutumia na kuibua masuala mapya kwa kuegemea katika matokeo ya utafiti huu.